Saturday, June 29, 2013

Haijawahi kutokea duniani, Nigeria ndiyo ya kwanza

Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Nigeria (NFF) Aminu Maigari amesema kuanzia sasa kocha wa timu ya taifa wa nchi hiyo hatakuwa na mamlaka ya kuchagua kikosi cha timu hiyo peke yake, bali shirikisho hilo litafanya kazi ya uteuzi wa kikosi cha timu ya taifa na kocha atakuwa anatoa ushari tu. Maigari amesema hayo, baada ya Nigeria kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la bara kwa kile kinachosemekana kucheza kikosi kibovu wakati Nigeria ina wachezaji wengi wazuri ambao wangeweza kuifikisha timu hiyo nusu fainali au fainali. Maamuzi haya ya shirikisho la Nigeria yatakuwa ni ya kwanza kutokea kwenye historia ya soka duniani, kwani duniani kote makocha ndiyo wenye mamlaka ya kuchagua kikosi cha timu wanayoifundisha na sio mtu mwingine. Je maamuzi haya ya NFF ni sahihi kufanya?? Ila wadau wengi wa soka ndani na nje ya Nigeria wamesema uamuzi huu wa NFF sio sahihi, kwani ni bora kumfukuza kocha kama hana uwezo wa kuifundisha timu kuliko kumtolea uhuru wa kuchagua kikosi anachokitaka. 

No comments:

Post a Comment