Sunday, February 2, 2014

Yanga wavunja rekodi ya Mbeya City ligi kuu

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo imevunja mwiko wa timu ya Mbeya City kucheza michezo ya Ligi bila kufungwa baada ya kuichapa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mrisho Ngasa ndiye aliyewapatia goli Young Africans katika dakika ya 16 ya mchezo baada ya kugongeana vizuri na kiungo Haruna Niyonzima na David Luhende.  

Young Africans: 1.Dida, 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo "Chumvi", 7.Saimon Msuva, 8.Haruna Niyonzima, 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kiiza, 10.Mrisho Ngasa, 11.David Luhende

Mbeya City: 1.David Burhani, 2.John Kabanda, 3.Hassan mwasapili, 4.Deogratias Julius, 5.Yusuf Abdallah, 6.Anthony Matogolo, 7.Mwigane Yeya, 8.Steven Mazanda, 9.Paul Nonga/Richard Peter, 10.Peter Mapunda/Stephen Wilson, 11. Deus Kaseke/Saad Kapanga

No comments:

Post a Comment