Baada ya kumaliza ziara yake kwenye mji wa Nagoya nchini Japan, klabu ya Arsenal ilipanda treni kuelekea mji mwingine wa Saitama ambapo wakiwa huko watacheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Urawa Red Diamonds. Treni hii ambayo wachezaji wa Arsenal wamepanda, ni treni inayokimbia kwa kasi kuliko zote duniani kwa spidi ya 200 M/H. Kutokana na sifa yake ya kwenda kasi, treni hii inajulikana kwa jina la The Bullet.
|
The bullet ikiwasili Nagoya ambapo timu itapanda kuelekea Saitama. Ikiwa Saitama klabu ya Arsenal inatarajia kushinda mechi yao ya mwisho ili kuendeleza rekodi nzuri ya ushindi waliyojiwekea tokea waanze ziara nchi za Asia. Baada ya kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Urawa, wachezaji na viongozi wa Arsenal watarejea nyumbani London tayari kujiandaa na michuano ya Emirates Cup. |
Walcott akimwaga wino |
Wachezaji wakiwa wamejiachia ndani ya The bulett |
Laurent Koscielny na Olivier Giroud wakiwa kwenye pozi la picha. |
No comments:
Post a Comment