Friday, July 19, 2013

Arsenal yatuma ofa ya mwisho kumsajili Suarez

Big money: Arsene Wenger has been given the green light to spend £40m on Luis Suarez
Sportsmail limethibitisha kuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekubali klabu yake kupeleka ofa ya paundi mil 40 kwa klabu ya Liverpool ili kumsajili Luis Suarez. Habari zinasema, Arsenal wameamua kutoa ofa hiyo ya mwisho kwa Liverpool kutokana na ukweli kwamba usajili wa Rooney na Higuain una ugumu kuliko wa Suarez. Hii ni ofa ya pili kupelekwa baada ya kukataliwa ofa ya mwanzo ambayo ilikuwa ni paundi mil 30. Sportsmail pia limethibitisha kukubaliwa kwa ofa hiyo na uongozi wa Liverpool ili iweze kujadiliwa. Wakati haya yakiendelea England, nchini Indonesia ambapo timu ya Liverpool ipo hivi sasa kwa ziara, kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers ameendelea na msimamo wake ule ule kuwa Suarez hauzwi kwa gharama yoyote, licha ya kuwa wakala wake, Pere Guardiola ameiomba klabu ya Liverpool kukubali mchezaji huyo kuhama ili aweze kutimiza mahitaji yake. Kama ofa hii ya Arsenal itakubalika basi Suarez atakuwa ndiye mchezaji ghali kuliko wote waliowahi kusajiliwa na klabu hiyo. 

No comments:

Post a Comment