Friday, July 19, 2013

'Tutarajie habari nzuri kuhusu Cesc' - Moyes

Optimist: David Moyes is hopeful over a transfer move for Cesc Fabregas
Klabu ya Man utd ina matumaini ya kumsajili kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas ndani ya masaa 48. Hayo yamethibitishwa na kocha wa Man utd, David Moyes alipokuwa akiongea na waandishi wa habari asubuhi ya leo nchini Australia. Moyes alisema ‘naamini tutawapa habari nzuri hivi karibuni, kwasasa, mkurugenzi mtendaji wa klabu yupo England anafuatilia suala hili, huwa nawasiliana naye kila wakati, na pindi atakapofanikiwa atanijulisha mara moja. Tunajitahidi kutekeleza haya ili tuimarishe kikosi chetu kwa kuongeza nguvu mpya. Kwasasa sina habari mpya ila baada ya siku chache nitakuja na habari nzuri’. Hayo ni maneno ya Moyes alipoulizwa kuhusu suala la Cesc Fabregas. Man utd ilituma maombi ya kumsajili Cesc siku tatu zilizopita kwa dau la paundi mil 26 na imesemekana mazungumzo yamefikia mahali pazuri baina ya Man utd na Barca kwa kutegemea ndani ya wikiendi hii usajili wa Cesc uwe umeshakamilika.

No comments:

Post a Comment