Friday, July 26, 2013

Azam TV kuonesha live mechi 60 ligi kuu

Kampuni ya SSB kupitia channel yake ya TV ijulikanayo kwa jina la Azam TV imeingia mkataba na TFF wa kuonesha Live mechi zote za ligi kuu Tanzania bara kwa misimu mitatu mfululizo. Azam TV imelipa kiasi cha Tsh Bilioni 6 ambapo kila klabu ya ligi kuu itapata fungu lake kutoka kwenye fedha hizi. Taarifa kutoka TFF zinasema Azam TV itaonesha mechi zipatazo 60 live na nyingine zitarudiwa kulingana na mahitaji ya mechi husika. Azam TV imefanikiwa kupata tenda hii baada ya kuipiku kampuni ya Super Sport ya Afrika kusini ambayo pia ilikuwa inahitaji kuonesha mechi hizi. Mbali ya ugeni katika habari, lakini Azam TV imetajwa kuwa na vyombo vipya na vya kisasa kuzidi vituo vingine vya Television nchini katika kuchukua na kurusha Live matukio, hivyo Watanzania watarajie ubora wa hali ya juu wa masafa kutoka Azam Tv. Kuonekana Live kwa mechi za ligi kuu Tanzania bara msimu ujao kutawafanya Watanzania waweze kuwajua vyema wachezaji wa ligi nyumbani na pia itarudisha umaarufu na ushabiki wa ligi ya nyumbani. Ligi kuu ya Tanzania bara inatarajia kuanza Agosti 24. 

No comments:

Post a Comment