FT | Everton | 2 - 0 | Manchester City |
FT | Aston Villa | 3 - 2 | Queens Park Rangers |
FT | Southampton | 3 - 1 | Liverpool |
FT | Stoke | 0 - 0 | West Bromwich Albion |
FT | Swansea | 0 - 2 | Arsenal |
Man united & Man City
Kwa matokeo haya, Man United imeendelea kufunguliwa njia ya kuchukua ubingwa. Mpaka sasa Man United ipo mbele kwa pointi 12 zaidi ya Man City. Leo usiku Man United atacheza na Reading, mechi ambayo inaonekana ni nyepesi kwa Man United licha ya kuwa Reading wanahitaji pia pointi ili kuepuka kushuka daraja.
Arsenal
Katika mechi ya leo, Arsenal amezidi kujiimarisha kutetea nafasi yake ya kushiriki kombe la mabingwa kwani amefikisha pointi 48 tofauti ya pointi 4 na Chelsea, licha ya kuwa Chelsea ana mchezo mmoja mkononi. Ili Arsenal aweze kushiriki ligi ya mabingwa atahitajika kushinda michezo mingi zaidi, ili apate nafasi ya tatu au ya nne. Kocha Arsene Wenger bado yupo kwenye wakati mgumu kwani msimu huu Arsenal imeshakosa makombe yote iliyokuwa ikigombea. Kocha Wenger amekuwa akipata malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki wa Arsenal wakimtaka abadilishe sera zake za kusajili. Lakini Wenger amekuwa mgumu kukubali kubadilika kwa kile anachoamini yeye kuwa wachezaji alionao wanamfaa. Uongozi wa Arsenal pia unapata wakati mgumu kumtoa Arsene kwani ni kocha ambaye ameipatia Arsenal mafanikio makubwa sana hasa ya kiuchumi na vilevile inasemekana Arsene Wenger anamiliki hisa katika timu hiyo. Mbali na haya, Arsene Wenger bado ni kocha mzuri na anaaminika duniani kote kama ni kocha anayeweza kumfundisha mchezaji kuanzia kwenye msingi hadi anakuwa mchezaji mwenye kiwango, mfano Cesc, Nasri na Kolo
No comments:
Post a Comment