Friday, July 12, 2013

Guardiola aanzisha bifu na Rais wa Barcelona

Preparations: Guardiola was speaking at Bayern's pre-season training camp in Arco, Italy
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ameanzisha bifu na Rais wa klabu ya Barcelona baada ya jana kumponda wakati akiongea na waandishi wa habari nchini Italia. Guadiola alimuongelea Rais wa Barca baada ya kuulizwa kuhusiana mahusiano yake ya sasa na kocha ya Barca, Pep alisema 'Baada ya kumaliza kazi ya kuifundisha Barcelona, mimi na familia yangu tulikwenda nchini Marekani ili tukapate mapumziko na kujiepusha na mambo ya soka. Nilifanya uamuzi huu ili niwe mbali kabisa na klabu ya Barcelona, lakini wao Rais wa klabu pamoja na mkurugenzi wa soka wa klabu walikuwa wakinitafuta na nilikuwa najitahidi kuwakwepa. Nimesikia wakiongea mambo mengi sana, zaidi wakisema, tokea Tito Vilanova (kocha wa Barcelona anayeumwa kansa) aanze kuumwa mimi sijawahi kwenda kumuona hospitali. Ni kweli sikwenda kutokana na sababu zilizokuwa juu ya uwezo wangu, lakini wao viongozi wa Barcelona wanatumia jambo hili ili kuleta ugomvi kati yangu mimi na Tito. Hawa watu ni waongo na wanatumia ugonjwa Tito vibaya, kama niliwahi kuwakera na jambo lolote ni bora wajitokeze waliseme, ila sio kutumia ugonjwa wa mtu kunikandamiza na kunianzishia ugomvi na mtu tunaye heshimiana. Siwezi kuongelea kwa udani zaidi lakini kwa yote yaliyotokea mimi nawatakia kila la heri'. Kufuatia taarifa hizi za Guardiola, uongozi wa klabu ya Barcelona kupitia makamu wake wa Rais Jordi Cardoner wamesema klabu ya Barcelona imesikitishwa sana na taarifa hizi, na Rais wa Barca ataliongelea suala hili hivi karibuni ili kuweka kila kitu wazi. Guardiola alimaliza mkataba wake na Barcelona mwaka 2012 na aliondoka Barca bila ya kufukuzwa huku kukiwa na maneno ya chini chini kuwa Guardiola alikuwa hapendani na Rais wa klabu hiyo Andro Rosell ndiyo maana aliamua kuondoka.  

Picha hii inawaonesha Pep Guardiola na Rosell (rais wa Barca) wakiwa kwenye mabishano mbele ya watu kipindi Pep akiwa kocha wa Barca licha ya kuwa haikujulikana walikuwa wakibishana kitu gani.

No comments:

Post a Comment