Friday, July 12, 2013

'Naongea na LS7 kila siku' - Kocha wa Liverpool

Kufuatia tetesi zilizopo kuhusu Luis Suarez kutaka kuhama Liverpool, Talksport TV ya Uingereza ilimtafuta kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ili kujua ukweli halisi wa jambo hili. Rodgers alijibu kwa kusema, ‘hata mimi pia nasoma taarifa hizi, lakini binafsi naongea na Suarez kila siku na hajawahi kuniambia suala hili. Suarez ni mchezaji mzuri, na kama Liverpool bado tunamhitaji. Kila siku lazima niwasiliana naye kwa meseji au kuongea naye kwani naamini neno langu moja kwake kwa kuongea au kumtumia ujumbe mfupi linaweza kubadilisha mawazo yake kama atakuwa anafikiria kuhama. Suarez bado ana mkataba wa miaka mitatu na sisi, hatuwezi kumuuza muda huu. Najua anapenda kucheza kwenye klabu zenye mafanikio zaidi ya Liverpool, lakini bado usajili unaendelea na nitasajili baadhi ya wachezaji wazuri ambao wataifanya Liverpool irudi kwenye hadhi yake na naamini Suarez atapenda kuendelea kuwa na sisi kwa msimu ujao’. Hadi sasa klabu za Arsenal na Real Madrid ndiyo zimeonesha nia ya kumsajili Suarez. Suarez bado yupo kwenye mapumziko baada ya kushiriki michuano ya kombe la mabara nchini Brazil na anatarajiwa kujiunga na wenzake tarehe 21 Julai. 

No comments:

Post a Comment