Friday, July 12, 2013

Wenger asema suala la usajili wa Suarez ni siri

Kocha mkuu wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger leo amegoma kuongelea chochote kuhusu usajili wa Luis Suarez baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari nchini Indonesia kama Arsenal ipo tayari kuongeza dau la usajili wa mchezaji huyo hadi kufikia paundi mil 40, Wenger alijibu swali hili kwa kifupi akiwa serious kwa kusema ‘kama mnavyojua, masuala ya usajili yanahitaji usiri wa hali ya juu sana, hivyo sipo tayari kuongea chochote kuhusiana na jambo hili’. Waandishi walimuuliza Wenger swali hili kufuatia tetesi zilizopo kuwa Arsenal ipo kwenye mazungumzo na Suarez baada ya mchezaji huyo kuonesha nia ya kuhama Liverpool. Licha ya kuwa Wenger hakujibu chochote kuhusiana na Suarez, lakini, wachambuzi wa masuala ya soka wamesema kauli ya Wenger imeonesha wazi kuwa klabu ya Arsenal ipo kwenye harakati ya kumsajili mshambuliaji huyo, kwani ni kawaida ya makocha wengi kutamka wazi kama hawana mpango wa kumsajili mchezaji, lakini kitendo cha Wenger kutaka jambo hili la siri imeonesha kuwa ni kweli Arsenal wapo kwenye harakati za kumsajili LS7. Arsenal wamefikia uamuzi wa kutafuta saini ya Suarez baada ya usajili wa Higuain kuonekana kuwa na ugumu sababu zikielezwa kuwa Madrid wanahitaji dau kubwa. Klabu ya Arsenal ipo nchini Indonesia kwa mara ya kwanza na inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa la nchini hiyo jumapili ya tarehe 14 kabla ya kuelekea nchini Vietnam na Japan. 

Fire away: Walcott, Wilshere, Wenger and Gazidis hold a packed press conference in Indonesia
Wenger akiwa anaongea mbele ya waandishi wa habari nchini Indonesia 

We're here: Arsenal boss Wenger presented with Indonesian attire as the team lands in Jakarta Culture: Walcott is getting in the spirit for the Asia tour
Wenger na Theo wakiwa wenye furaha baada ya kutua nchini Indonesia na kupokelewa kwa upendo na mashabiki wa Arsenal.  

No comments:

Post a Comment