Tuesday, July 2, 2013

Kaseja bado ni golikipa wa Taifa Stars - Poulsen

Kocha wa timu ya taifa (Taifa stars) Kim Poulsen amesema Juma Kaseja ataendelea kuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa hata kama ametemwa na klabu yake ya Simba. Poulsen ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati anatangaza kikosi cha Stars kitakachooingia kambini kesho kujiandaa na michuano ya CHAN. Poulsen alisema 'Kuhusu Kaseja na Simba mimi hayanihusu na wala sijui undani wake kuzidi nyinyi (waandishi). Kaseja bado ni mchezaji mzuri na kiwango chake ni kizuri, hivyo ataendelea kuwa mchezaji wa Stars na nahodha wa timu ya taifa kama kawaida, na natarajia kumuona kesho kwenye mazoezi ili kujiandaa na mechi dhidi ya Uganda'. Kaseja ambaye alikuwa ni golikipa nambari moja wa klabu ya Simba, wiki iliyopita klabu yake ilitangaza rasmi kumtema mchezaji huyo kwasababu kwamba mkataba wake umekwisha na klabu ya Simba haikuwa tayari kusaini mkataba mpya na mchezaji huyo. Kwasasa Kaseja yupo mkoani Kigoma akifanya mazoezi binafsi kama mchezaji huru. 

No comments:

Post a Comment