Tuesday, July 9, 2013

Kaseja njia nyeupe kujiunga na Mtibwa Sugar

Baada ya uongozi wa klabu ya Coastal Union kutamka wazi kuwa hawana mpango wa kumsajili aliyekuwa golikipa namba moja wa klabu ya Simba, Juma Kaseja, tetesi zimeibuka kuwa mchezaji huyu huenda akajiunga na klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. Akizungumza na Mwananachi kocha mkuu wa Mtibwa, Meck Mexime, amesema 'milango ipo wazi kwa Kaseja kujiunga na klabu ya Mtibwa pindi golikipa wetu Mohamed Sharifu atafanikiwa kusajiliwa na klabu ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokorasia ya Congo'. Licha ya kuwa Sharifu bado hajasajiliwa na Limpopo, lakini usajili huu unaonesha kufanikiwa na upo kwenye hatua za mwisho mwisho. Taarifa hizi zitakuwa ni njema kwa kocha wa timu ya taifa Kim Poulsen ambaye ameonesha kumuamini sana Kaseja, hivyo angependa kumuona anaendelea kucheza kwenye klabu kubwa nchini ili aweze kudumu kwenye timu ya taifa. Hadi sasa Kaseja bado hana timu yoyote tokea mkataba wake na klabu ya Simba kumalizika.

No comments:

Post a Comment