Hatimaye mshambuliaji wa Barcelona, David Villa atua Atletico Madrid kwa dau la paundi mil 4.5. Mtakaba wa Villa kwenda At. Madrid bado unahusisha umiliki wa 50% kwa Barcelona na mchezaji huyu atakapouzwa au kuleta mafanikio yoyote kwa At Madrid au kuuzwa, 50% ya mapato au ada ya uhamisho itarudi kwa Barcelona. Usajili wa Villa kwenda At. Madrid umekuwa wa kushitukiza kwani mchezaji huyu alikuwa ametajwa kuhusishwa na klabu za Tottenham na Arsenal. Hivyo kwa taarifa hizi, Tottenham na Arsenal itabidi zihamishie majeshi yake ya usajili kwingine. Villa alijiunga na Barca mwaka 2010 ameshacheza mechi 119 na kufanikiwa kufunga magoli 48. |
Monday, July 8, 2013
David Villa asajiliwa na Atletico Madrid
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment