Wacheza wa zamani wa Man utd (David Beckham, Ryan Giggs, Gary Neville, Phil Neville, Nicky Butt na Paul Scholes) walikutana jumatatu ya wiki hii kula bata pamoja na kukumbushana mambo ya enzi hizo. Wachezaji hawa walikutana Man utd tokea mwaka 1992 na walianza kuvuma sana miaka ya 1997 hadi 2010. Kutokana na mafanikio waliyoyapata wakiwa na Man utd, wachezaji hawa hadi leo bado ni mabalozi wazuri klabu yao, na zaidi pia kwa Giggs na P.Neville ambao wamechaguliwa kuwa makocha wasaidizi wa klabu. Haya ni moja ya matunda ya kocha mstaafu Sir Alex ambayo yameanza kuinufaisha klabu kwa mara ya pili, kwani ni klabu chache sana zilizofanikiwa kuwatunza na kufunda wachezaji wake hadi wakaweza kufikia hatua ya kuwa makocha ndani ya klabu zao. Kwa hili Man utd wanastahili pongezi.....
|
No comments:
Post a Comment