Mchezaji tegemezi wa Tottenham Gareth Bale, leo ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake jambo ambalo linaashiria kuendelea kuwepo Enfield msimu ujao. Klabu ya Real Madrid imekuwa ikimwinda Bale tokea msimu wa ligi kuisha, lakini hadi sasa klabu hiyo haijafanikiwa kumsajili mchezaji huyu. AVB, kocha mkuu wa Tottenham ndiye aliyemshinikiza Bale kubaki Tottenham na jitihada zake zimeonekana kufanikiwa. Katika kufanikisha hili, AVB aliwezesha Bale kuongezewa mshabara hadi kufikia paundi 130,000 kwa wiki, baada ya kuomba uongozi wa Tottenham kufanya hivyo ili kumbakisha mchezaji huyo. Uwepo wa Bale pamoja na mchezaji mpya Mbrazili, Paulinho, kutaifanya klabu hii kuwa madhubitu zaidi na inatarajiwa kuleta changamoto zaidi kwa klabu kubwa katika kunyang'anyiro cha kombe la ligi na FA msimu ujao. |
Monday, July 8, 2013
Madrid basi tena, Bale aanza mazoezi na Tottenham
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment