Malumbano yameibuka kwa wadau wa soka baada ya Real Madrid kutoa jezi yao mpya ya ugenini ambayo imefanana na jezi ya Chelsea. Jezi hizi mpya za Madrid zinatofauti ya majina ya wadhamini na logo za klabu tu dhidi ya zile za klabu ya Chelsea. Haijajulikana hadi sasa kama klabu ya Chelsea itaichukulia hatua kampuni ya Adidas ambao ni watengenezaji wa jezi hizi au walishakubaliana tokea mwanzo. Ila wadau wengi wamesema klabu ya Chelsea ina haki ya kushitaki au kulipwa kwani yenyewe ndiyo inamiliki haki ya mtindo na rangi ya aina hii ya jezi. |
Friday, July 26, 2013
Madrid watoa jezi za ugenini kama za Chelsea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment