Wednesday, July 17, 2013

Man utd yaitolea nje Chelsea kwa mara ya pili

Something on your mind? Wayne Rooney arrives at Manchester United's training ground on Wednesday
Klabu ya Chelsea leo imetolewa nje kwa mara ya pili na Man utd kumsajili Wayne Rooney. Sportsmail limeripoti kuwa, klabu ya Chelsea imetoa ofa ya paundi mil 10 pamoja na mchezaji mmoja kati ya Mata au Luiz ili kumsajili Rooney, lakini Man utd wameitolea nje ofa hiyo na kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo sio wa kuuzwa. Katika kusisitiza msimamo wake, Man utd wameiomba klabu ya Chelsea kutopeleka maombi mara ya tatu kwani mchezaji huyo hawezi kuondoka United kwa gharama yoyote. Wakati Chelsea wanakutana kibuti, klabu ya Arsenal pia imeripotiwa kujiandaa kutoa ofa nyingine kwa United ili kumsajili mchezaji huyo, ofa ambayo imesemekana itakataliwa pia. Klabu hizi mbili zimekuwa zikiwasilisha ofa zao kwa United ili kumsajili Rooney kwa kile kinachosemekana kuwa Rooney mwenyewe hataki kubaki Man utd, licha ya kuwa klabu yake bado inamuhitaji. Muda wa usajili bado upo lolote linaweza kutokea…

No comments:

Post a Comment