Friday, July 12, 2013

Moyes afunguka mara ya mwisho 'Rooney hauzwi'

Kocha wa Man utd, David Moyes leo mchana ameongea kwa mara ya mwisho kuhusu tetesi zilizopo kuwa Wayne Rooney atahama United msimu huu. Moyes ameongea hayo akiwa nchini Thailand baada ya mwandishi mmoja kumuuliza kuhusiana na taarifa kwamba Rooney anarudi nyumbani ili kufanikisha uhamisho wake kwenda Chelsea huku akinukuu maneno ya Jose Mourinho aliyoyasema kuwa anampenda mchezaji huyo na angependa awe pamoja na Chelsea, Moyes alisema ‘nahishi sikueleweka wiki zilizopita nilipoongelea swala la Rooney, narudia tena kwa mara ya mwisho, Rooney sio mchezaji wa kuuzwa na ataendelea kuwa mchezaji wa Man utd. Kuhusu Jose Mourinho sio kawaida kuongelea wachezaji wa timu nyingine, ila kama atakuwa amesema kuhusu Rooney itakuwa ni maoni yake tu’. Wakati Moyes akisema hayo, Rooney ameshawasili nchini Uingereza leo asubuhi akitokea Thailand baada ya kuumia jana mchana akiwa kwenye mazoezi na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mzima. Man utd kesho itacheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Singha All Stars kwenye uwanja wa Rajamangala nchini Thailand.   
Direct approach: Jose Mourinho has admitted he likes Wayne Rooney 'very much'
Rooney akiwa amezungukwa na baadhi ya maofisa wa Man utd pamoja na polisi baada ya kutua nchini Uingereza leo asubuhi akitokea Thailand. 

No comments:

Post a Comment