Saturday, July 6, 2013

Yanga ziarani kutembeza kombe kanda ya ziwa

Wachezaji na baadhi ya viongozi wa klabu ya Yanga wakiwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mji mwanza leo jioni katika ziara yao ya kulitembeza kombe la ubingwa mikoani. Mbali ya ziara hiyo, klabu ya Yanga pia imecheza mechi ya kirafiki dhidi ya KCC ya Uganda na matokeo ya mwisho yalikuwa ni droo ya goli 1-1. Kikosi cha Yanga leo kiliwakilishwa na Yusuph Abdul,Juma Abdul,Oscar Joshua, Rajab Zahir, Mbuyu Twite, Salim Telela, Nizar Khalfani, Hamis Thabit , Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, Abdallah Mnguli 'Messi'

No comments:

Post a Comment