Saturday, July 6, 2013

Bartoli bingwa wa Wimbledon 2013 wanawake

First of many? Marion Bartoli beat Sabine Lisicki to grab her first ever grand slam title
Marion Bartoli akiwa ameshikilia ngao yake baada ya kushinda mechi ya fainali ya Wimbledon dhidi ya Sabine Lisicki  kwa seti mbili mfululizo za 6-1, 6-4. Hii ni mara ya kwanza kwa Bartoli kushinda kombe hili, na leo itakuwa ni siku ya  kihistoria katika maisha yake. Mbali ya ushindi huu wa Bartoli, Wimbledon ya mwaka huu ilishuhudia wakongwe wengi ambao walitarajiwa kutwaa kombe hili kutolewa katika roundi za awali akiwemo Serena, Maria Sharapova, Na Li, na Carlone W. Kutolewa kwa wakongwe hawa kumeifanya michuano hii ipoteze raha yake kwa vile walioingia fainali (Bartoli na Lisicki) ni wachezaji waliokuwa na mashabiki wachache, licha ya kucheza mchezo safi wa kuvutia tokea raundi ya tatu hadi fainali. Fainali ya wanaume itafanyika kesho jumapili ambapo Djokovic atapambana na mwenyeji Murray. 
Until next year: Lisicki, who overcame Serena Williams in the fourth round, had to settle for second
Lisicki akinyanyua ngao yake kama mshindi wa pili huku machozi yakimlenga kwa kukosa ubingwa kwani anajua inaweza kumchukua miaka mingi hadi kufika fainali tena. Lisicki ndiye alimtoa bingwa wa michuano hii Serena Williams
Sabine Lisicki  Marion Bartoli

No comments:

Post a Comment