Monday, June 3, 2013

Arsenal imevunja mkataba na Denilson

Denilson has left the Emirates after seven years at the club (©GettyImages)
Klabu ya Arsenal imemtema rasmi kiungo wake Denilson ambaye alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja. Denilson (25) msimu uliopita alikuwa anacheza kwa mkopo kwenye klabu ya Sao Paulo nchini Brazil, licha kupata nafasi ya kucheza kwenye mechi nyingi na Sao Paulo lakini kiwango chake bado kimekuwa cha chini kulingana na mahitaji ya Arsenal, hivyo Arsenal ikafikia uamuzi wa kuvunja mkataba wake na tayari wakala wa Denilson ameshatangaza kwa timu yoyote inayomuhitaji itume maombi kwani ni mchezaji huru kwasasa. Denilson alijiunga na Arsenal mwaka 2006 akitokea Sao Paulo na amecheza mechi 150 tu kwa kipindi chote cha miaka saba kwenye klabu ya Arsenal. 

No comments:

Post a Comment