Wednesday, August 7, 2013

Barcelona wajipanga kutuma ofa ya pili kwa Luiz

David Luiz
Klabu ya Barcelona imeendelea na jitihada za kutafuta saini ya beki wa Chelsea, David Luiz kwa mara ya pili baada ya kutakatiliwa ofa ya kwanza. Sportmail limeripoti kuwa, mkurugenzi wa soka wa klabu ya Barcelona, Raul Sanllehi ameshawasili jijini London kuongea na wakala wa Luiz kabla ya kutuma ofa ya pili. Haijajulikana klabu ya Barcelona imejipanga kutoa ofa ya paundi ngapi kwa mara ya pili, lakini klabu ya Chelsea imesema mchezaji huyu hatauzwa chini ya paundi mil 40, ikiwa ni tofauti ya paundi mil 19 ya ile aliyonunuliwa nayo mwaka 2011 akitokea Benfica. 

No comments:

Post a Comment