Wednesday, August 7, 2013

Ribery, Messi na Ronaldo waingia tatu bora ya UEFA

Wachezaji watatu Lionel Messi, Franck Ribery na Cristiano Ronaldo wameingia kwenye hatua ya tatu bora kuchagua mchezaji bora wa UEFA mwaka huu. Wachezaji hawa wamechagulia kutoka kwenye kundi wa wachezaji kumi lililokuwa limewajumuisha Bale, Ibrahimovic, Lewandowski, Muller, Schweinsteiger, Robben, na RVP. Sifa za wachezaji hawa watatu walioingia tatu bora zinatofautiana, ambapo Ribery ameshinda makombe mawili, Uefa champions na kombe ligi, Messi ameshinda kombe la ligi na mfungaji bora wa ligi kwa magoli 46 wakati Ronaldo ni mfungaji bora wa Uefa magoli 12. UEFA itamtangaza mshindi tarehe 29 Agosti siku ambayo makundi ya UEFA champions pia yatapangwa. 

No comments:

Post a Comment