Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa mshambuliaji wake Lionel Messi ni majeruhi baada ya kupata maumivu kwenye paja lake la mguu wa kushoto. Messi alipatwa na maumivu hayo kwenye mechi ya jana usiku dhidi ya Atletico Madrid, mechi ambayo ilikwisha kwa droo ya goli 1-1. Kocha wa Barcelona Tata Martino alisema Messi alitolewa baada ya mapumziko ili kuepusha kuumia zaidi kwani alianza kulalamika kujisikia maumivu tokea mwanzo wa mchezo. Uongozi wa klabu ya Barcelona kupitia tovuti yake umesema Messi anatarajia kufanyiwa vipimo leo na baada ya vipimo itajulikana ukubwa wa tatizo alilonalo. Ila taarifa za awali zinasema Messi ataweza kukosa mechi kadhaa za wiki mbili zijazo. |
Thursday, August 22, 2013
Messi majeruhi, kufanyiwa vipimo leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment