Tuesday, June 18, 2013

Kesi ya Ribery na Zahia kuendelea Juni 26

Kesi ya kiungo wa Bayern Munich Frank Ribery leo tena imeendelea mahakamani baada ya kutuhumiwa kutoka na kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa chini ya miaka 18 Zahia Dehar. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili hakimu wa kesi hii alitoa muda kwa uchunguzi zaidi na tarehe 26 mwezi huu kesi hiyo itasomwa tena na kutolewa hukumu. Kabla ya kughairisha kesi, wakili wa serikali ambaye anasimama kwa niaba na Zahia (binti), alisema Zahia alikuwa anasafiri kwa ndege kutoka Ufaransa hadi Ujerumani kufanya mapenzi na Ribery na alikuwa anamlipa Zahia Euro 700 kila akilala naye, kipindi hicho Zahia alikuwa na umri wa miaka 16. Akijibu hoja hiyo, wakili wa Ribery, alikiri kuwa mteja wake (Ribery) alifanya kitendo hicho, lakini hoja za Ribery ni kwamba binti huyo alimdanganya umri wake, alisema ana umri juu ya miaka 18 na alikutana naye klabu akinywa pombe maeneo ambayo si ruhusa kuingia mtu yoyote aliyechini ya umri wa miaka 18. Pia Zahia alikuwa anajihusisha na biashara ya kujiuza shughuli ambazo zinatakiwa kufanywa na mtu juu ya miaka 18. Hivyo, kutokana na hoja za Ribery, inaonesha kuwa Ribery ataweza kushinda kesi licha ya kuwa kesi hii imemfanya apoteze heshima yake kwa jamii na familia yake. Ribery mwenye mke na watoto watatu kama atashindwa kesi hii itabidi aende jela kwa miaka mitatu au kulipa faini ya paundi 40,000.    

Jet setter: Zahia Dehar worked as a prostitute when she was underage
Zahia msichana aliyekuwa akitoka na Ribery akiwa katika pozi
Zahia Dehar Zahia Dehar
 
Picha mbalimbali za Zahia 

No comments:

Post a Comment