Wednesday, August 21, 2013

Yanga kukata rufaa adhabu ya Mrisho Ngassa

Klabu ya Yanga imesema itapeleka barua TFF kukata rufaa kwa adhabu iliyopewa kuhusu usajili wa Mrisho Ngassa. Klabu ya Yanga imefikia uamuzi huo baada ya mchezaji wake Mrisho Ngassa kupewa adhabu ya kulipa faini ya mil 45 na kufungiwa kucheza mechi kadhaa. Akielezea jambo hili mbele ya waandishi wa habari katibu mkuu wa klabu ya Yanga Lawrence Mwalusako alisema ‘tunawaandikia barua TFF kukata rufaa dhidi ya adhabu tuliyopewa kuhusu Ngassa kwani hatujaelewa kwanini tumepewa adhabu hii, kwasababu tulifuata taratibu zote za usajili. Kama Ngassa na Simba walipewana wenyewe pesa kwa kukubaliana, basi sualla hili litakuwa ni la mchezaji mwenyewe na klabu ya Simba, hivyo haliwezi kutuhusu sisi kama Yanga. Sisi kama klabu tunaweza kufanya utaratibu wa kulitatua ila sio kuhusishwa moja kwa moja’. Mwalusako alisema barua hiyo ipo tayari na inategemea kufikishwa TFF muda wowote. Kwa mujibu wa barua ya TFF Ngassa anatakiwa kulipa mil 45 na hataruhusiwa kucheza mechi sita kutokana na kusaini mkataba na Yanga akiwa bado mchezaji wa Simba. Kama atashindwa kulipa fedha hizo, hataruhusiwa kucheza mechi yoyote ya ligi msimu mzima. 

No comments:

Post a Comment