Saturday, August 3, 2013

Mourinho amponda tena Cristiano Ronaldo, amesema mwenye jina ni Ronaldo wa Brazil

Tried and failed: Mourinho asked the Real board to sign Bale last summer
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amemponda tena Cristano Ronaldo baada ya kusema mchezaji huyu sio orijino, na kumtaja Ronaldo de Lima wa Brazil kuwa ndiye Ronaldo orijino mwenye jina. Mourinho alitoa kauli hii alipokuwa akihojiwa na ESPN jana mchana akisema ‘ mwaka 2000 ndiyo ilikuwa mwanzo wangu kufundisha klabu kama kocha mkuu, lakini kabla ya hapo nilishafundisha klabu kubwa na wachezaji wakubwa nikiwa kama kocha msaidizi. Nimeshawahi kumfundisha Ronaldo, sio huyu mnayemjua nyinyi, bali ni yule orijino, Ronaldo wa Brazil, ambaye ndiye mwenye jina lake’. Mourinho alitoa kauli hii ili kuonesha uzoefu wake huku akimponda Cristiano Ronaldo, mchezaji ambaye alikaririwa akimuita mjuaji asiyefundishika. Kauli hii ya Mourinho imeendelea kuonesha chuki aliyonayo kwa mchezaji huyu na amekuwa akimuongelea kwa ubaya mara kadhaa tokea ahame Madrid. Mbali ya hili, Mourinho pia aliongelea suala la usajili wa Bale na kusema, ‘ Bale ni mchezaji mzuri, niliomba kumsajili tokea nikiwa Real Madrid, lakini niliambiwa muda wa kumsajili bado. Naamini huu ndiyo muda mzuri wa kusajiliwa, nitafurahi kumuona Bale akichezea Real Madrid kwasababu ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee atakayeisadia Madrid’.  

Mourinho anamuita huyu ni Ronaldo orijino, akimaanisha kuwa ndiye mmiliki wa jina Ronaldo kwenye tasnia ya soka na sio Cristiano Ronaldo. Mourinho alimtaja Ronaldo de Lima kuwa ni mchezaji mwenye heshima na msikivu ndiyo maana alidumu na kupata mafanikio makubwa.
Superstar: A three-pronged attack with Real Madrid forward Cristiano Ronaldo would be tough to stop
Mourinho anamuita huyu Ronaldo jina tu. Maana kubwa ya Mourinho ni kusema Cristiano Ronaldo anatumia mgongo wa jina la Ronaldo de Lima.  

No comments:

Post a Comment