Tuesday, August 20, 2013

Neville na Carragher waipasha klabu ya Arsenal

Gary Neville
'Hakuna mchezaji wa Arsenal anayeweza kusema matatizo ya klabu yaliyopo sasa, lakini, ukweli ni kwamba klabu ya Arsenal jinsi ilivyosasa inahitaji kusajili wachezaji wasiopungua watano. Nililisema hili mwishoni mwa msimu uliopita na sasa ndiyo linatakiwa kutekelezwa ila Arsenal wameshachelewa. Kwa muda uliobakia wa wiki mbili haiwezekani kupata mchezaji unayemtaka, Arsenal ilitakiwa kutekeleza zoezi la usajili mapema ili kuepuka matatizo yanayowakabili muda huu'.

Jamie Carragher
'Kwasasa wanataka kumsajili Cabaye, kama kweli Cabaye alikuwa ni chaguo lao, wangeanza harakati za kumsajili tokea zamani. Kitendo cha kuanza kumhangaikia Cabaye muda huu ni dalili tosha zinazoonesha Arsenal wamechanganyikiwa. Mimi sio mshabiki wa Arsenal, lakini, ninaumia kama vile nashabikia Arsenal, najua Wenger hawezi kufanya usajili wowote wa maana kwa muda uliobakia. Ukweli ni kwamba, washabiki wa Arsenal wanaipenda sana klabu yao, na wananunua tiketi kwa wingi kuliko klabu yoyote England, lakini uongozi timu ndiyo unawaangusha'. 

No comments:

Post a Comment