Thursday, June 27, 2013

Sahara Marathon, mbio ngumu kuliko zote

Mbio za kilomita 220 za Jangwa la Sahara ndiyo ngumu kuliko zote duniani. Mbio hizi zinashirikisha wakimbiaji kutoka nchi zaidi ya 50 duniani kote. Mbio za Sahara zinazojulikana kwa jina maarufu “Highway to hell” hufanyika katika nchi ya Morocco kila mwaka ikishirikisha wakiambiaji zaidi ya 1,000 wakike kwa wakiume. Ugumu wa mbio hizi, wakimbiaji wanatakiwa kukimbia kwa kilomita 220 kwa kutumia siku saba. 
Washiriki wa mbio za Sahara wakikatisha kwenye jangwa kukiwa na jua kali, upepo na joto lililofika digrii 50

Mshiriki akikatisha kwenye vilima vidogo vidogo vyenye mchanga mzito

Washiriki wakipandisha mojawapo ya mlima mrefu katika mbio hizo
Mbio hizi zina historia ya kusababisha vifo vya watu watatu kutokana na hali mbaya ya hewa inayofikia digrii 50 zikiambatana na vumbi zito lenye upepo na jua kali. Sheria za mchezo huu kila mshiriki anatakiwa kukimbia bila kupumzika kilomita 75 kwa masaa 34, akiwa amebeba chakula, maji na baadhi ya vifaa vya kumsaidia kukimbia visivyopungua kilo tano.

No comments:

Post a Comment