Monday, August 19, 2013

Chelsea kutuma ofa ya mwisho kumsajili Rooney

Destination unknown: Rooney pictured on the bench, watching as his colleagues took charge of the game
Baada ya Wayne Rooney kuonekana hana raha kwenye mechi kati ya Man utd na Swansea jumamosi iliyopita, klabu ya Chelsea imejipanga kutuma ofa ya mwisho kwa Man utd ili kumsajili mchezaji huyu. Chelsea imepata nguvu ya kutuma ofa ya mwisho kutokana na ukweli kwamba Rooney mwenyewe ameonesha hali ya kutofurahia maisha yake akiwa United. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, amethibitisha nia ya Chelsea ya kutaka kutuma ofa ya mwisho akisema ‘kikosi changu kwasasa kinapungukiwa na mtu mmoja tu naye ni Rooney, tutafanya kila tuwezalo hadi dakika ya mwisho kuhakikisha Rooney anakuja Chelsea ili kikosi chetu kiwe imara zaidi’. Ofa ya mwisho ya Chelsea itakuwa ni paundi mil 40 na mkataba wa miaka minne ikiwa sambamba na malipo ya paundi 300,000 kwa wiki. 

No comments:

Post a Comment