Friday, September 6, 2013

Real Madrid walimtosa Neymar mwaka 2005

Hii ni fomu ya Neymar aliyoitumia kufanya majaribio ya kuichezea Real Madrid mwaka 2005, lakini baada ya kufanyiwa majaribio mkurugenzi wa Madrid wakati huo Carlos Martínez alikataa kumnunua Neymar kwa Euro 60,000 akisema pesa hizi ni nyingi kulingana na uwezo wa mchezaji mwenyewe. Kitendo hiki cha kumkataa Neymar kiliwafanya Madrid wajutie baada ya mchezaji huyu kuibuka mwaka 2010 akionekana mwenye kipaji cha hali ya juu. Lakini jitihada za Madrid kumrudisha Neymar ziligonga mwamba baada ya Neymar mwenyewe kuichagua Barcelona.

Video Neymar akiwa Madrid mwaka 2005 kwenye majaribio 

No comments:

Post a Comment