Friday, September 6, 2013

Casillas apewa majukumu ya Uefa champions

Gazeti namba moja kwa michezo nchini Hispania 'Marca' limeripoti kuwa kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, ameshatatua kitendawili cha nafasi ya golikipa kilichokuwepo kati ya Casillas na Lopez. Marca limeripoti kuwa Ancelotti amemwambia Casillas atakuwa akidaka kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya (Uefa champions league) na golikipa namba mbili Giego Lopez atakuwa akidaka kwenye mechi za ligi kuu nchini Hispania. Uamuzi huu wa Ancelotti utamfanya Casillas azidi kushuka kiwango, kwani katika michuano ya Uefa Champions Casillas atacheza mechi zisizopungua 10 kwa msimu mmoja kama Real Madrid itafika fainali. 

No comments:

Post a Comment