Monday, October 28, 2013

Afrika kuongeza timu za kombe la dunia 2018

UEFA president Michel Platini
Platini, Rais wa UEFA akiongea mbele ya waandishi wa habari juu ya uwakilishi wa timu za Afrika na Asia kwenye kombe la dunia mwaka 2018. Platini amesema anapenda timu ziongezeke kutoka 32 hadi 40 ili kila kundi liwe na timu tano badala ya nne. Katika mapendekezo yake Patini amesema timu anazopenda ziongezwe ni kutoka Afrika na Asia. Kwasasa Afrika inawakilishwa na timu tano na Asia inawakilishwa na timu nne. 
FIFA President Sepp Blatter has threatened to slash European and South American teams to get more sides from Africa and Asia at the World Cup
Rais wa FIFA Sepp Blatter akiongelea juu ya uwakilishi wa kombe la dunia, maoni yake yamekuwa tofauti na Platini kuhusu idadi ya timu. Blatter alisema ' nakubaliana na Platini kuhusu kuongezwa kwa timu kutoka Afrika na Asia, lakini mimi mawazo yangu ni kupunguza timu kutoka Ulaya na kuongeza timu kutoka Asia na Afrika ili kuweka uwiano unao karibiana kwenye uwakilishi'. Kwasasa Ulaya inatoa timu 13 kwenda kombe la dunia, ikiwa ndiyo bara lenye timu nyingi kuliko mabara yote. 

No comments:

Post a Comment