Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amekabidhi leseni B kwa makocha walioshiriki kozi iliyofanyika mjini Zanzibar mwaka jana.
Jamhuri Kihwelo alipokea leseni hiyo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa niaba ya washiriki wengine tisa waliofuzu mafunzo hayo.
Makocha wengine waliofuzu kozi hiyo iliyoendeshwa na mkufunzi Bhekisisa Boy Mkhonta kutoka Swaziland ni Abdulghan Msoma, Hafidh Badru, Nasra Juma Mohamed, Gulam Abdallah Rashid, Mohamed Ayoub Suleiman, Shaaban Ramadhan, John Simkoko na Hemed Suleiman Ali.
Hivi sasa Tanzania ina makocha 40 wenye leseni B za CAF baada ya wengine 31 kufuzu katika mafunzo yaliyofanyika mapema mwaka juzi jijini Dar es Salaam chini ya mkufunzi Honor Janza kutoka Zambia.
No comments:
Post a Comment