Monday, October 21, 2013

Baines amkimbiza Evra Manchester United

Staying or going? Patrice Evra seems destined to leave Manchester United
Beki tegemezi wa kushoto wa Man utd Patrice Evra ametangaza kuondoka Man utd mwishoni mwa msimu huu pindi mkataba wake utakapomalizika. Evra aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari akisema ' nafikiria kufikia kikomo kuichezea Man utd mwisho wa msimu huu. Nimeamua kuondoka kwasababu zangu binafsi na sio kama vile watu wanavyosema, lakini siwezi kuzisema ni sababu zipi. Man utd wananitaka niendelee kuwepo, lakini mimi nimeona basi'. Wachambuzi wa masuala ya soka pamoja na waandishi wa habari wanasema uamuzi huu wa Evra umesababishwa na kustaafu kwa Sir Alex pamoja na nia ya Man utd ya kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines, jambo ambalo limemfanya Evra ajihisi kuwa hana mchango kwasasa ndani ya klabu. 
Target: Manchester United wanted to bring in Leighton Baines who may have displaced Evra
Leighton Baines (kulia), mchezaji anayewindwa na Man utd, imesekana anaweza kusajiliwa kwenye dirisha dogo
Blow: Evra was also sad that legendary manager Sir Alex Ferguson left the club
Sir Alex ndiye sababu kubwa inayomfanya Evra kuondoka, kwani Moyes ameonekana kutokumkubali Evra. 

No comments:

Post a Comment