Pichani ni wachezaji na viongozi wa klabu ya Man utd wakiwasili kwenye uwanja wa Cologne nchini Ujerumani baada ya hekaheka angani. Hekaheka hiyo ilitokea wakati ndege ya shirika la Monarch iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Man utd kushindwa kutua kutokana na uwepo wa ndege nyingi kwenye sehemu iliyotakiwa kutua. Pailoti alifanya uamuzi wa kughairisha kutua akiwa mita 400 jambo ambalo limeelezwa kuwa ilikuwa ni hatari. Kutokana na hali hii ndege hiyo ililazimika kuchelewa kwa dakika kumi kutoka muda iliyotakiwa kutua. Hatari ya tukio hili ingeweza kusababisha ndege iliyokuwa imebeba wachezaji kugongana na nyingine au kutua nje ya uwanja. Baada ya ndege kutua pailoti alikwenda kwenye chumba cha abiria na kuwaomba samahani viongozi na wachezaji wa Man utd kwa hekaheka iliyotokea. Man utd wanatarajia kucheza na Bayer Leverkusen usiku wa leo kwenye mechi za Uefa champions.
No comments:
Post a Comment