Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo pamoja na refa aliyechezesha mchezo kati ya Madrid na Bilbao, Miguel Angel wamepewa adhabu na shirikisho la mpira la nchini Hispania. Ronaldo amepewa adhabu ya kulipa faini paundi 1000 pamoja na kukaa nje ya uwanja mechi tatu baada ya kusababisha vurugu uwanjani na kutembea polepole wakati akitoka nje wa uwanja. Refa Miguel yeye amepewa adhabu ya kutochezesha mechi za Madrid msimu huu pamoja na kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja baada ya kushindwa kumudu vyema mchezo huo.
Miguel alimpa Ronaldo kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Madrid na Bilbao wikiendi iliyopita baada ya kumparua usoni kiungo wa Bilbao.
Ronaldo akitembea taratibu baada ya kupewa kadi nyekundu, jambo hili la kupoteza muda ndilo limemfanya apewe adhabu na shirikisho la mpira wa miguu nchini Hispania.
No comments:
Post a Comment