Monday, December 30, 2013

Arsenal na mipango ya kumsajili Morata wa Madrid

Handy acquisition: Real Madrid youngster Alvaro Morata could do a number of jobs for Arsenal if released
Klabu ya Arsenal imetajwa kumchukua mshambuliaji wa Real Madrid Morata kwa mkopo. Taarifa hizi zimeeandikwa sana wikiendi hii na magazeti mbalimbali ya michezo nchini England na Hispania. Taarifa hizi zinasema kuwa klabu ya Arsenal ipo kwenye hatua za mwisho kumtathimini Morata ili kama itawezekana mwezi January 2014 achukuliwe kwa mkopo. Uamuzi huu umekuja ili kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Arsenal ambayo imeonekana butu. Awali, klabu ya Arsenal ilikuwa imsajili mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez, lakini kitendo cha mchezaji huyu kuongeza mkataba na klabu yake kumeondoka kabisa matumaini ya Arsenal kumsajili ndani ya dirisha dogo. Kwasasa klabu ya Arsenal inawategemea Olivier Giroud na Nicklas Bendtner kwenye safu ya ushambuliaji ambao wanacheza chini ya kiwango hali inayosababisha wafungaji wakubwa wa Arsenal kuwa viungo.

No comments:

Post a Comment