Tuesday, December 31, 2013

Messi yupo fiti anatarajia kurudi dimbani Jan 5

Messi gets back to work in Argentina
Maendeleo ya Lionel Messi yameleta matumaini makubwa kwa benchi la ufundi na madaktari wa klabu ya Barcelona baada vipimo kuonesha mifupa kujiunga. Kabla ya kufanyiwa vipimo wiki hii, madatari wa timu walisema Messi atarudi dimbani tarehe 11 January, lakini baada ya vipimo vya wiki hii madaktari wamethibitisha kuwa Messi atarudi dimbani tarehe 5 na anatarajia kucheza dhidi ya Elche. Taarifa ya Marca inasema, jitihada zaidi ya kupoma mchezaji huyu imeongezeka baada ya kocha wa Barca Tata Martino kuwajulisha madaktari umuhimu wa Messi kwenye mechi dhidi ya Atletico Madrid inayotarajiwa kuchezwa jijini Madrid tarehe 11 January. Kwasasa Messi anafanya mazoezi ya kumrudisha kwenye hali ya mchezo ili aweze kucheza mechi ya tarehe 5. Messi anatarajiwa kurudi Barcelona tarehe 2 January akitokea nchini Argentina. 

No comments:

Post a Comment