Wednesday, January 29, 2014

Hali ya Michael Schumacher bado tete hospitali


Mashabiki wa Michael Schumacher wakiwa nje ya hospitali aliyolazwa, huku wakipeperusha bendera siku ya birthday ya Schumacher. 

Mwezi mmoja umepita tokea Michael Schumacher kujeruhiwa katika ajali ya mchezo wa kuteleza kwenye barafu. Meneja wa Schumacher ameiambia BBC kwamba madaktari wanaendelea kumpatia matibabu katika uangalizi mkubwa na kwamba yuko katika hali nafuu kuliko awali. Bingwa huyo mara saba aligonga kichwa chake kwenye mwamba wakati akiteleza kwenye barafu katika milima ya Alps nchini Ufaransa. Madaktari wanatumia madawa ya usingizi ili kumpunguzia uvimbe na kuchubuka kwenye ubongo wake. Michael Schumacher tayari ameshapasuliwa mara mbili kuondoa damu iliyoganda kwenye ubongo. Hata hivyo huenda maisha yake yakawa hatarini iwapo ataendelea kuwa katika hali ya kuzirai kutokana na hatari ya ubongo wake kuharibika na kupata maambukizi ya kifua.

No comments:

Post a Comment