Kocha Jose Mourinho na Mata wakionesheana uso wa mbuzi baada ya mchezaji huyu kutolewa dakika ya 53 ya mchezo kati ya Southampton na Chelsea. Mata alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Oscar. Mabadiliko haya ndiyo ilikuwa chachu ya ushindi wa Chelsea dhidi ya Southampton. Baada ya mechi kuisha, Mourinho alihojiwa kuhusu Mata na alisema mchezaji huyu yupo huru kuondoka kwasababu Oscar na Hazard wanamchango mkubwa kumzidi. Mbali ya Mata, Mourinho pia alimgusia Essien na kusema mchezaji huyu pia yupo huru kuondoka. Maneno haya ya Jose yametoa mwanya kwa vilabu mbalimbali barani Ulaya ambavyo vilikuwa vinamhitaji Mata. Hadi sasa klabu ambazo zimetajwa kumsajili Mata kwenye dirisha dogo ni PSG, Arsenal na Tottenham. Chini kuna Video unaweza kuziangalia ili kupata story kamili.
Essien akimtuliza Mata baada ya kutolewa dakika ya 53
Video: Mata akilalamika baada ya kutolewa
Vidoe Mourinho akiongelewa suala la Mata
No comments:
Post a Comment