Friday, January 24, 2014

Wachezaji waliouzwa kimakosa na klabu zao

Daniel Sturridge ni moja ya wachezaji ambao wameuzwa kwa hasara na klabu zao. Sturridge aliuzwa na klabu ya Chelsea akiwa kama mchezaji asiyekuwa na faida, lakini tokea ahamie klabu ya Liverpool, Sturridge ameweza kuonesha kiwango cha hali ya juu jambo ambalo limemfanya kufunga magoli 11 akiwa amecheza mechi 14 za ligi kuu hadi sasa. Sturridge alipatwa na majeraha yaliyomfanya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi, jambo ambalo lilimfanya azidiwe kwa magoli na wachezaji wengine baada ya kushikiria takwimu za ufungaji bora wa EPL tokea ligi ianze. Kiwango cha hali ya juu cha mchezaji huyu hakika ni majuto kwa klabu ya Chelsea iliyomuuza kwa bei ya kutupa. 

Mesut Ozil alihamia klabu ya Arsenal akitokea Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita. Ozil uwezo wake unajulikana tokea akiwa kwenye ligi ya Ujerumani na sasa yupo klabu ya Arsenal akicheza nafasi ya kiungo kwa ufanisi mkubwa. Moja ya chachu ya mafanikio ya klabu ya Arsenal ndani ya msimu huu ni Mesut Ozil ambaye ameweza kwa kiasi kikubwa kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji kwenye timu ya Arsenal. Ozil pia ameongeza sana hamasa na motisha ya wachezaji na washabiki wa klabu ya Arsenal, kwani ni miaka mingi klabu ya Arsenal haijasajili mchezaji mwenye jina kubwa jambo ambalo liliwakatisha tamaa wachezaji na washabiki. Hadi sasa klabu ya Arsenal inashikilia nafasi ya kwanza kwenye ligi na Ozil amewezesha kufungwa magoli 7 wakati yeye ameshafunga magoli manne. Katika kuthibitisha kuwa uhamisho wa Ozil ulikuwa ni hasara kwa Madrid, vurugu kubwa za mashabiki wa Madrid zilizuka siku Gareth Bale alipotambulishwa kwa mashabiki wa klabu hiyo kwani walikuwa hawataki mchezaji huyu kuuzwa. Mashabiki wa Madrid walisikika wakimzomea Rais wa klabu baada ya kumuuza Ozil, lakini pia kocha wa Madrid Carlos Ancelotti alikiri kufanya makosa kumuuza mchezaji huyu.  

Click next to see the ten selected players (©GettyImages)
Robben aliuzwa na klabu ya Chelsea kwenda Real Madrid na Madrid walimuuza kwenda Bayern Munich, ni miaka mingi imepita tokea mchezaji huyu ahame kutoka Chelsea na Madrid, lakini uwezo wake kwasasa ni mkubwa mnoo. Robben ndiye alikuwa mchezaji tegemezi wa Bayern Munich msimu uliopita, msimu ambao ulikuwa ni historia kubwa ya mafanikio kwa klabu ya Bayern Munich baada ya kushinda makombe yote makubwa ya klabu ikiwemo kombe la ligi, Uefa champions na kombe la dunia la vilabu. Hadi sasa mchezaji huyu ni moto wa kuotea mbali na anategemea kuiongoza nchi yake Holland kwenye kombe la dunia. Wanasoka wanakubali kuwa mchezaji huyu kama angekuwepo kwenye klabu za Chelsea au Madrid hadi sasa bado angekuwa ni mchango mkubwa wa kuleta ushindi. 

No comments:

Post a Comment