Ligi kuu ya England imeshakuwa na wachezaji wengi wazuri waliokuwa wanaifanya ligi inoge zaidi. Wachezaji hawa wengi walisajiliwa na klabu vigogo kwa pesa nyingi na wengine waliondoka kutokana na mahusiano mabaya yaliyojitokeza baina yao na makocha au uongozi wa klabu. Matokeo ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji hawa hadi leo washabiki wa ligi ya England wanawakumbuka. Ifuatayo ni orodha wachezaji tisa (9) ambao walihama England lakini bado wanakumbukwa kutokana na umahiri wao ndani ya klabu walizokuwa wakicheza.
9. Luka Modric
Modric alihama kutoka Tottenham kwenda Real Madrid kwa paundi mil 30 mwaka 2012. Anakumbukwa kwa magoli ya mbali na kumiliki mpira vyema kwenye nafasi ya kiungo.
8.Arjen Robben
Robben alihama Chelsea kwenda Real Madrid kwa paundi mil 15 mwaka 2007, anakumbukwa kwa counter attack, magoli ya mbali na kuwakimbiza mabeki.
7.Carlos Tevez
Tevez alihama Man city kwenda Juventus mwaka 2013, anakumbukwa kwa magoli ya kushitukiza na kashikashi langoni mwa adui.
6.Xabi Alonso
Mashabiki wa Liverpool wanamkumbuka Alonso hadi leo, alihamia Real Madrid mwaka 2009. Alonso anakumbukwa kwa magoli ya mbali, pasi ndefu na mashuti makali
5.Mario Balotelli
Mario alihama kutoka Man city kwenda Ac Milan, anakumbukwa kwa vituko ndani na nje wa uwanja ikiwemo magoli makini ya bila kutumia nguvu.
4.Didier Drogba
Drogba alihama Chelsea kwenda klabu ya Shaghai mwaka 2012, atakumbukwa daima na washabiki wa Chelsea kwa kufunga magoli muhimu, kuwapa kashikashi mabeki wa timu pinzani na pia alikuwa na uwezo wa hali ya juu kufunga magoli ya vichwa.
3.Gareth Bale
Bale alihama kutoka Tottenham kwenda Real Madrid kwa paundi mil 85 mwaka 2013. Bale ndiye alikuwa tishio la mabeki wa EPL, alikuwa na uwezo wa kuwapita mabeki wa timu pinzani kilaini akitumia mbio na ndiye aliyekuwa tegemeo la Tottenham kwa counter attack.
2.Cesc Fabregas
Cesc alihama Arsenal kwenda Barcelona mwaka 2011 kwa paundi mil 35. Cesc atakumbukwa kwa kumiliki mipira, kupiga pasi nzuri na kufunga magoli ya muhimu kwa Arsenal.
1.Cristiano Ronaldo
Ronaldo ndiye mchezaji anayekumbukwa kuliko wote EPL aliyehama kutoka Man utd kwenda Real Madrid kwa paundi mil 80. Ronaldo anakumbukwa kwa kuwa mfungaji bora mara kwa mara, kupiga chenga, faulo nzuri na kujituma uwanjani.
No comments:
Post a Comment