Wednesday, February 26, 2014

Ter Stegen afanyiwa vipimo vya siri na Barcelona

Kipa wa Borussia Mönchengladbach, Ter Stegen ameshapita vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Barcelona. Stegen alifanya vipimo hivyo kwa siri ndani ya klabu ya Barcelona na ameshasaini mkataba wa awali wa kujiunga na klabu hiyo mwisho wa msimu. Klabu ya Borussia Monchengladbach imeshatangaza kuwa Stergen atajiunga na Barcelona mwisho wa msimu. Stergen atajiunga na Barcelona kwa Euro mil 9 ili kuziba pengo la kipa wa sasa wa Barcelona Victor Valdes ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu. 

No comments:

Post a Comment