Saturday, March 1, 2014

Vita ya Yanga na Azam TV



Taarifa ya Azam TV ilianza hivi..........

Tumepokea maswali na simu nyingi sana zikiuliza kama Azam TV itaonesha mechi kati ya Yanga na Al Ahal leo, jibu ni kwamba HAPANA... Ukweli ni kwamba tulipokea maombi toka kwa agent aliyenunua pambano kwa niaba ya Watu wa Misri ambaye aliomba Azam TV impe gharama za kuzalisha ili kuweza kupeleka feed yenye ubora wa kimataifa North Africa & Middle East na ikiwezekana kuonesha nchini Tanzania. Katika vikao vyote na Agent, Azam TV iliweka wazi kuwa ipo tayari kuzalisha bure na hata kama ikibidi kuonesha delayed sawa kwa kuwa Yanga walionesha wazi kuzuia Live Coverage nchini kwa kuhofia mapato kupungua. 

Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam TV na kuamua kutoa pesa waliyolipwa kukilipa kituo kimoja nchini ambacho ndicho kilichopewa kandarasi kwa malipo licha ya kutokidhi vigezo vya watu wa Egypt ambao walitaka angalau 8 Cameras OB na Azam TV iliwapa 10 Cameras OB with HD Feed. Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu wateja wetu kuwa Azam TV ilikuwa tayari kuwapa Yanga na Agent ushirikiano wote ili pesa yote waliyopewa na Watu wa Misri iingie klabuni lakini wao wameamua kuitumia kulipia production iliyo sub-standard ili mradi tuu kuinyima fursa Azam TV. Pamoja na haya yote Azam TV inaitakia kila la kheri klabu ya Yanga kwenye mchezo wake wa leo, na inaamini matatizo hayapo kati ya Azam na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja mwenye nguvu ndani ya Yanga


Taarifa ya Yanga ikajibu hivi....

Naona Kazi imebakia kuisema Young Africans vibaya, SGM waliingia mkataba na Yanga, Yanga nao walichagua kituo cha kufanya nacho kazi, sasa tunashangazwa na Taarifa zinazoenezwa kwamba tumekataa kuwapa wao nafasi ya kuonyesha mpira leo. Kama wana uhakika na wanachokisema waonyeshe barua ya hao waliowaomba kutumia kituo chao kuonyesha mchezo wa leo. Walianza na kusema wameombwa Uwanja wa mazoezi, Balozi wa Misri akakanusha na kuleta barua ya maombi ya uwanja kwetu tukashirikiana nao kupata IST. Hivyo ni bora tukawa tunatoa taarifa zenye uhakika wa maandishi kama ni kweli kudhibitisha kauli hizo, vinginevyo ni kuendelea kujipunguzia thamani kwa taarifa za Uongo.

No comments:

Post a Comment