Saturday, March 8, 2014

Yanga yawasili Alexandria tayari kwa mchezo

Msafara wa kikosi cha Young Africans umewasili salama jijini Alexandria leo majira ya saa 7 na kufikia katika hoteli ya Shaeraton ukitokea katika jiji la Cairo ambako awali mchezo wa marudiano ulipangwa kufanyikwa kabla ya jana kutolewa mabadiliko ya uwanja na mchezo huo utachezwa kesho katika dimba la Uwanja wa El Max Stadium jijini Alexandria.

Young Africans ambayo iliwasili juzi jijini Cairo na kuweka kambi katika hoteli ya Nile Paradise Inn na kufanya mazoezi kwa siku mbili mfululizo katika uwanja uliopo ndani ya hoteli hiyo ambayo uongozi wa Young Africans kwa kushirikiana na Ubalozi uliweza kufanikisha kambi hiyo.

Awali makamu mwenyekiti wa Young Africans Clement Sanga alitangulia jijini Alexandria jana asubuhi pamoja na maofisa wa ubalozi kwa ajili ya kufanya maaandalizi ya sehemu ambapo timu itafikia na leo timu ilipofika ilikuta kila kitu kmeshakaa kwenye mpangilio wake. 

Mara baada ya kuwasili jijini Alexandria wachezaji na viongozi wa Young Africans wamepata chakula cha mchana kisha wamepata mapumziko mpaka majira ya saa 12 jioni ambapo timu itakwenda uwanja wa El Max kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo huo.

 Morali ya wachezaji bado ni ya hali ya juu kuelekea mchezo huo wa kesho, haki ya kambi ni nzuri hakuna majeruhi hata mmoja hivyo vijana wote wapo tayari kwa kesho kuipeperusha bendera ya nchi.

Jioni timu itafanyya mazoezi katika Uwanja wa El Max ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa kesho. 

No comments:

Post a Comment