Klabu ya Arsenal imefanikiwa kufanya makubaliano ya awali na klabu ya Barcelona ili kumsajili Alexis Sanchez. Makubaliano haya yanahusisha ada ya uhamisho ya paundi mil 34, kama mipango itakwenda vyema, Alexis atajiunga rasmi na Arsenal ndani ya wiki hii.
Klabu ya Liverpool imetuma maombi kwa klabu ya Benfica ili kumsajili mshambuliaji wake, Lazar Markovic. Maombi ya Liverpool yamekuja baada ya Alexis Suchez wa Barcelona kugoma kujingu nao katika dili la kumnunua Suarez. Ada ambayo Liverpool inategemea kumsajili mshambuliaji huyu ni paundi mil 19.
Kiungo wa Ujerumani na Bayern Munich, Toni Kroos amesema atatoa jibu la klabu atakayochezea msimu ujao baada ya kombe la dunia. Mkataba wa Kroos na Munich unakwisha mwaka 2015 na tayari klabu ya Real Madrid imeshatuma maombi ya kutaka kumsajili mchezaji huyu. Vyombo vingi vya habari barani Ulaya vinasema Kroos tayari ameshasaini mkataba na Madrid na yupo tayari kujiunga na klabu hiyo kama Bayern Munich watakubali kumuuza.
Dailymail linaripoti kuwa klabu ya Man utd ipo tayari kutuma maombi kwa klabu ya Juventus ili kumsajili kiungo wake Arturo Vidal. Dailymail limesema Vidal ni moja ya chaguo la kocha mpya wa Man utd Louis van Gaal, hivyo maombi yankumsajili Vidal yanaweza kutumwa mapema wiki hii na kama ikiwezekana mchezaji huyu anaweza kusajiliwa kabla ya kombe la dunia kumalizika.
Eric Abdial ametua Olympiakos akitokea Monaco
Cole atua Roma akitokea Chelsea
Real Madrid ipo kwenye hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Colombia na Monaco, James Rodriguez.
The Mirror linaripoti kuwa klabu ya Man utd inafanya mipango ya kumsajili winga wa Argentina na Real Madrid Angel Di Maria kwa Euro 60mil. Winga huyu ametajwa kuwa ni chaguo la kwanza la kocha Van Gaal katika harakati zake za kutaka kuibadilisha United. Maombi ya kumsajili mchezaji huyu yanatarajiwa kutumwa baada kombe la dunia au baada ya Argentina kutoka kwenye michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment