Thursday, June 20, 2013

Thiago na mpira ulioandikwa tukutane Man utd

BNIkg24CAAI Cvu David De Gea signs Thiago Alcantaras matchball See you in Manchester
Baada ya mechi ya fainali ya U21 kuisha kati ya Hispania na Italia, mchezaji wa Hispania na Barcelona Thiago Alcantara alionekana amebeba mpira uliokuwa na maandishi ya Kihispania yakisema  "Nos Vemos en Manchester" yakiwa na maana  "tutakutana Manchester". Taarifa zinasema maneno hayo yameandikwa na moja ya wachezaji wa Hispania bila ya kutajwa jina lake, lakini ukweli ni kwamba David de Gea ndiye mchezaji pekee wa Man utd aliyopo kwenye timu hiyo ya Hispania. Thiago amekuwa akihusishwa kuhamia Man utd lakini klabu yake ya Barcelona bado inamshikilia asiondoke kwa kile kinachosemekana kuwa Thiago ndiye mrithi wa Xavi na Iniesta. Lakini hadi sasa, Thiago mwenyewe ameshaonesha nia ya kuhamia United ili aweze kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza tofauti na Barcelona ambapo mara zote anaanzia benchi. Msimu wa usajili bado unaendelea hivyo lolote linaweza kutokea na Thiago akajiunga na United. 

 David De Gea signs Thiago Alcantaras matchball See you in Manchester
Thiago alibeba mpira huu ikiwa ni kumbukumbu yake baada ya kufunga magoli matatu kwenye mechi hiyo ya fainali ambapo Hispania iliondoka na ushindi wa magoli 4-2 na kunyakuwa kombe la Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21. 

No comments:

Post a Comment