Tuesday, April 30, 2013
Maneno ya Jose Mourinho baada ya Madrid kutolewa
Baada ya mechi kuisha huku Real Madrid wakitolewa kwenye michuano ya UEFA Jose Mourinho alihojiwa kuhusiana na mechi na kusema, 'tumecheza vizuri sana, wachezaji wamecheza kwa nguvu moja
mwanzo hadi mwisho lakini siwezi kusahau mechi ya kwanza, tuliyocheza
Ujerumani, tulicheza vibaya sana, Dortmund walinipa adhabu kubwa mno na
tumetoka kwasababu ya adhabu ya goli 4-1. Vilevile nimesikitishwa sana na refa
wa leo hajatoa kadi kwenye faulo nyingi hususani penati tulizopata bila yeye
tungekuwa fainali muda huu. Alipoulizwa kuhusu uwepo wake Real Madrid msimu
ujao Mourinho alisema, napenda kuwepo mahali ambapo watu wananipenda na
wanafurahia uwepo wangu kwahivyo nitakuwepo mahali ninapopendwa, ikiwa ni
ishara ya wazi kabisa kuwa msimu huu ndiyo mwisho wake Real Madrid kwani watu
wa Real wamekuwa wakimponda sana Mourinho wakisema amewaharibia mpira wao.
Real Madrid wametolewa kiume kwa magoli 3-4 BVB
Timu ya Real Madrid imetolewa kwenye michuano ya UEFA champions na Dortmund baada ya ushindi wa magoli finyu 2-0 hivyo kuiwezesha Dortmund kusonga mbele na kuingia fainali kwa jumla wa magoli 4-3. Real Madrid ilicheza mchezo mzuri wa kuvutia na kwa kasi kubwa tokea mwanzo hadi mwisho wa mchezo lakini safu yake ya ushambuliaji haikuwa makini kumalizia mipira ya mwisho. Cristiano Ronaldo, Higuain, Ozil, Kaka na Di Maria wamechezea nafasi nyingi sana ambazo kama wangezitumia vizuri basi Real Madrid wangeweza kutoka kifua mbele kwa magoli mengi. Golikipa wa Dortmund pia alionesha umahiri wake mkubwa sana baada ya kuokoa mipira mingi ambayo ilikuwa ni magoli ya wazi. Katika mahojiano kabla ya mechi Jose Mourinho kocha wa Real Madrid alisema watakwenda kupigana kufa na kupona na kucheza kwenye kiwango chao cha juu kuliko siku zote, ni kweli wachezaji wa Real wametekeleza aliyosema Jose lakini umahiri wa mabeki wa Dortmund ndiyo umeifanya timu hiyo iweze kuhimili mikiki ya Real Madrid. Hivyo hadi mwisho wa mchezo Real Madrid 3-4 Dortmund. Mchezo mwingine wa nusu fainali utachezwa leo usiku jumatano kati ya Barcelona na Bayern Munich, ikiwa pia ni mchezo wa "mission impossible" kwa Barcelona kwani watahitajika kuwafunga Bayern magoli matano kwa bila ili wafuzu jambo ambalo matokeo yake yanawezekana kimahesabu kuliko kiuhalisia. Magoli yalifungwa na Benzema 83, Sergio Ramos 89.
Vikosi vya timu zote mbili
Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Ramos, Varane, Coentrao (Kaka 57); Xabi Alonso (Khedira 67), Modric; Di María, Özil, Cristiano Ronaldo, Higuaín (Benzema 57)
Borussia Dortmund: Weidenfeller; Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer; Bender (Santana 90), Gundogan; Gotze (Grosskreutz 14), Reus, Blaszczykowski; Lewandowski (Kehl 87)
![]() |
Benzema na Ramos wakishangilia goli la kwanza la Real Madrid lililogungwa na Benzema dakika ya 83 |
![]() |
Ronaldo, Benzema na Ozil wakigombania mpira dhidi ya goli kipa wa Dortmund baada ya goli la kwanza kufungwa, golikipa wa Dortmund aling'ang'ania mpira ili kupoteza muda |
![]() |
Ronaldo akinyoosha mikono kuomba penati baada ya kuangushwa katika dakika ya 92 ya mchezo, lakini refa hakutoa penati kwasababu aliangushwa hakiwa bila mpira |
![]() |
Mourinho akishangaa pia kufuatia kitendo cha refa kugomea penati baada ya Ronaldo kuangushwa chini dakika ya 92 |
![]() |
Cristiano Ronaldo akitoka nje wa uwanja kwa masikitiko baada ya mchezo kumalizika kwa matokeo ya jumla Real Madrid 3-4 Dortmund |
![]() |
Vita ilikuwa kali kati ya Ramos na Lewandowski, katika mchezo uliopita Jose Mourinho alisema mabeki wake hawamkufanyia rafu za kutosha Lewandowski ndiyo maana aliwafunga magoli mengi, akasema mchezo wa marudiano vijana wake watamchezea rafu za kutosha Lewandowski kitu ambacho walikitekeleza, ikiwemo kumpiga viwiko, kumkanyaga na kumsukuma |
Jason Collins ajitangaza rasmi kuwa ni shoga
Mchezaji wa Washington Wizards Jason Collins ametangaza
rasmi kuwa yeye ni shoga baada ya uvumi wa muda mrefu. Jason alijitangaza kwenye jarida la Sports Illustrated lililomnukuu akisema ‘Mimi
nina umri wa miaka 34, mchezaji mweusi wa NBA ni shoga’, taarifa hizi
zimelipuka kwenye vyombo vya habari nchini Marekani kwani sio jambo la kawaida
kwa mchezaji wa NBA kujitangaza hadharani kuhusu ushoga. Jason katika mahojiano
na ABC News leo asubuhi amesema, baada ya kujitangaza hadharani anajisikia kuwa
huru na mwenye furaha sana. Kufuatia kauli hiyo ya kujiweka hadharani, watu
wengi maarufu nchini Marekani akiwemo
rais mstaafu Bill Clinton na mchezaji mwenzake Kobe Bryant wamempongeza Jason kwa
uamuzi wake na wametoa ombi kwa wachezaji wengine kufuata nyayo za Jason. Lakini
uchambuzi umeonesha kuwa licha ya Marekani kuwa mbele kimaendeleo ya jamii
hususani uhuru wa kuongea na kudumisha haki za binadamu lakini bado itakuwa
vigumu kwa wachezaji wote ambao ni mashoga kujitangaza kwasababu wanahofia
kubaguliwa, kuzomewa na hata kukosa huduma zingine kama mashoga. Nchi nyingi
barani Ulaya na Amerika zimekuwa zikihamasisha kukubalika kwa ushoga ikiwa ni sera
za kisiasa ili kushinda chaguzi mbalimbali lakini ndani ya jamii zenyewe za wa
Amerika na Ulaya bado jambo hili la ushoga halijakubalika katika jamii yote.
Vilevile, jamii kubwa inachukulia mtu shoga kama ni dhaifu hivyo kwa
wanamichezo ambao wanatakiwa kuwa wakakamavu itakuwa vigumu sana kujitangaza kuwa ni mashoga kwani ajira zao zinaweza kuzorota na pia kupoteza mashabiki.
Jason Collins mwenye urefu wa futi 7 kabla ya kujiunga na Washington Wizards mwaka
huu ameshacheza kwenye timu kubwa za NBA zikiwemo Boston Celtics, Atlanta
Hawks, Memphis Grizzlies, Minnesota na New Jersey Nets.

TFF yatoa hati ya uhamisho kwa Yusuf
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji. Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza Ligi Kuu nchini humo. Kunasa ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent) amejiunga na timu hiyo akiwa mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji kumi kutoka Tanzania hivi sasa wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji. Timu ya Estrela Vemalha hadi sasa inashika nafasi ya kumi kwenye ligi ya msumbiji ikiwa imecheza mechi sita, imeshinda miwili, droo moja na imepoteza michezo mitatu sio timu kubwa nchini Msumbiji kwani ilishuka daraja mwaka 2008 na kwasasa ipo kwenye kipindi cha kujiimarisha kwani miaka ya 80 ilishawahi kuiwakilisha Msumbiji kwenye michuano ya Afrika pamoja na kushinda kikombe cha jijini la Mputo mwaka 2010.
Mechi za ligi kuu Tanzania bara wiki hii 1/5/13
Yanga Sc vs Coastal Union
Mtibwa Sugar vs African Lyon
Polisi Moro vs Kagera Sugar
JKT Ruvu vs Tanzania Prisons
Ruvu Shooting vs JKT Oljoro
Brandts,tutaendeleza ushindi mechi zilizosalia
Kocha mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema pamoja na kuwa tayari wameshatangazwa mabingwa wapya, bado kikosi chake kitashuka dimbani kuhakikisha kinaendeleza wimbi la ushindi wa kusaka pointi tatu katika michezo iliyosalia.Brandts alisema "Wengi wanaona kwa kuwa tumeshatwaa ubingwa basi tutapunguza kasi ya ushindi, hilo kwetu hakuna, tunaendelea na mazoezi kujiandaa kuhakikisha tunashinda michezo yote iliyosalia na kumaliza ligi kwa rekodi nzuri kuliko timu zote". Yanga inacheza na Coastal Union jumatano ya wiki hii, mchezo utakaovuta mashabiki wa Yanga kwa wingi ili kushangilia ubingwa, katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana jijini Tanga, Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union mabao yaliyofungwa na washambuliaji Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu. Mechi hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge kutoka Iringa.
Viingilio Yanga vs Coastal union
Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000 na tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo. Uongozi wa klabu ya Yanga umewaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wa timu ya Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya jumatano (mei mosi) katika dimba la uwanja wa Taifa ili kuishangilia timu yao na kuendeleza shangwe ya kutwaa Ubingwa wa VPL msimu huu.
Azam FC wameanza mazoezi leo Morocco
Azam FC imetua salama Casablanca Morocco na kusafiri kwa basi umbali wa kilometa 100 hadi Rabat wamefikia katika hoteli ya Golden Tulip mjini Rabat. Wakiwa mjini Rabat Azam leo asubuhi wameanza mazoezi kujiandaa na mechi yao dhidi ya AS FAR timu ambayo inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini Morocco nyuma kwa pointi sita dhidi ya vinara Raja Casablanca wenye pointi 56. AS FAR wamebakiza mechi sita msimu huu wa ligi lakini hadi sasa imefungwa michezo miwili tu na inategemewa kuchukua ubingwa wa Morocco kwani ipo nyuma kwa michezo miwili dhidi ya vinara wa ligi. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es salaam, Azam FC na AS FAR zilitoka droo ya bila kufungana hivyo basi Azam FC inatakiwa kutoka droo yoyote ya magoli au kushinda katika mchezo wake wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi wiki hii.
Tutacheza kiwango cha juu kuliko siku zote -Jose
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema leo watacheza
katika kiwango chao cha juu kuliko siku zote dhidi ya Dortmund ili kufuzu kwenda fainali. ‘Lazima tucheze
katika kiwango chetu cha mwisho, watu wanasema hatuwezi lakini sisi tunataka
kuonesha uwezo wetu, jambo hili linawezekana lakini lazima tuwe katika kiwango
chetu cha juu ndiyo tutaweza kushinda, hatuwezi kucheza kama tulivyocheza
Dortmund, siku ile kiwango chetu hakikuwa kizuri na mabeki wangu hawakuweza kumchezea rafu za kutosha Lewandowski, walimwachia ndiyo maana alituumiza, haiwezekani mchezaji acheze dakika tisini akufunge magoli manne na haujamfanyia rafu hata moja, mabeki wangu walikuwa wazembe, ila safari hii tumejipanga vyema’ hayo yalikuwa maneno ya Jose alipokuwa akihojiwa kusiana na mechi ya leo. Wakati huo huo Ronaldo aliyekuwa majeruhi akisumbuliwa na paja
ameruhusiwa na madaktari kucheza mechi ya leo akiwa ndiye mfungaji tegemezi wa
Madrid kwani ameshacheza mechi 11 na kufunga magoli 12 kwenye champions ligi.
Katika mechi ya leo “mission impossible” Real Madrid wanatakiwa kushinda magoli
matatu kwa bila au zaidi dhidi ya Dortmund ili iweze kufuzu kwenda fainali
baada ya kufungwa goli 4-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Monday, April 29, 2013
Yanga wanataka makofi ya heshima kwa Coastal
Msemaji wa Yanga bwana Baraka Kizuguto amesema klabu ya Yanga inahitaji kupigiwa makofi ya heshima kama mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara
mwaka huu. Klabu ya Yanga ambayo imeshatangazwa mabingwa ikiwa wamebakiza mechi
mbili, wamehitaji siku ya mechi yao inayofuata dhidi ya Coastal Union wachezaji
wa Coastal wapange mistari miwili huku wachezaji wa Yanga wakipita katikati kwa
kupigiwa makofi kama wananyofanya kwenye ligi za Ulaya. Kitendo hiki cha
kupigiwa makofi ya heshima ni kawaida kufanyika katika ligi za ulaya mfano Man
utd walipigiwa makofi na timu ya Arsenal katika mechi ya jumapili iliyopita
kama mabingwa wa ligi ya Uingereza mwaka huu. Lakini alipoulizwa katibu mkuu wa
TFF bwana Angetile Osiah kuhusiana na jambo hilo alisema Yanga
haitaweza kufanyia kitendo hicho kwasababu katiba ya sasa ya TFF hairuhusu
kufanya kitendo hicho kwahivyo itakuwa ni vigumu kwa Yanga kupewa heshima hiyo
na Coastal Union, ila bwana Osiah amesema jambo hilo ni zuri litazingatiwa ili
liwepo kwenye katiba ya TFF. Kitendo hiki cha kupiga makofi ya heshima
kimeanzia barani Ulaya ikiwa ni moja ya jitihada ya vyama vya soka duniani
kuhamasisha “fair play” hivyo TFF ni vyema wakalifanyia kazi jambo hili kwani
mashabiki wa soka Tanzania wanangojea kwa hamu kuona Simba au Yanga inampigia
makofi mwenzake, licha yakuwa tukio hilo litakuwa la kihistoria kwenye soka la
bongo.
![]() |
Tukio hili la kupigiwa makofi ya heshima lilitokea jumapili iliyopita Arsenal walipowapigia makofi Man utd kama mabingwa wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza, kitendo kama hiki ndicho Yanga wamehitaji kufanyiwa katika mechi yao inayokuja dhidi ya Coastal Union. |
Mwamuzi afungiwa kuchezesha maisha Russia
Mshika kibendera Musa Kadyrov wa nchini Urusi amefungiwa maisha
kuchezesha mechi nchini humo baada ya kumshambulia kwa ngumi na mateke mchezaji
wa Amkar Perm, Ilya Krichmar. Musa alifanya kitendo hicho mara tu mwamuzi wa kati kupuliza filimbi ya mwisho kumaliza mchezo. Kijana huyo aliyeshambuliwa alisema ‘ mshika kibendera huyu
amekuwa akichezesha vibaya mechi nyingi zikiwemo za kwetu, ila mimi sijawahi
kumsema vibaya popote, sasa sijui kwanini alinipiga mimi, nawashukuru wachezaji
wenzangu waliokuja kunisaidia, angeniumiza kwa hasira aliyokuwa nayo’. Matukio
kama haya ya waamuzi kuwapiga wachezaji ni nadra sana kutokea kwani wao
wanasimama kama wasuluhishi wa mchezo hivyo ni kosa kubwa kushiriki katika
kuvunja sheria za soka.
Video ya tukio hilo
Balotelli atoa kauli nzito kuhusu mpenzi wake
![]() |
Neguesha, mpenzi wa Balotelli |
Mshambuliaji wa Ac Milan Mario Balotelli ametoa kauli nzito baada ya kusema kwamba kama Real Madrid itashinda dhidi ya Dortmund
na kuingia fainali atawapatia wachezaji wa Real Madrid mpenzi wake. ‘Kama Real
Madrid watashinda magoli mengi na kuingia fainali Wembley basi
nitawaachia wachezaji wote wa Real Madrid watoke na mpenzi wangu Fanny Neguesha,
nasema hivi kwasababu najua Madrid hawatoki kwa Dortmund’ Mario ameyasema hayo
alipokuwa anaongea na gazeti la As Marca. Kauli hii ya Mario imetafsiriwa tofauti na wapenzi wa
soka wakisema amemdhalilisha mpenzi wake, kwani sio vyema
kufananisha utu au dhamani ya mwanadamu na vitu vya kupita. Ila mashabiki wa
Real Madrid nchini Hispania wameipokea kauli hiyo kama chachu ya ushindi, na
wamesema watakwenda Italia kumchukua usiku huo huo baada ya ushindi. Real
Madrid itashuka dimbani kesho April 30 kupambana na Dortmund katika mchezo wa
marudiano jijini Madrid, katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ujerumani, Dortmund
iliichapa Real Madrid goli 4-1, hivyo Madrid ipo kwenye wakati mgumu kwani
itahitajika kushinda magoli matatu kwa bila au zaidi ili kufuzu kuingia fainali.
Rage aviponda vilabu vya Tanzania
Mwenyekiti wa klabu ya Simba Isamil Aden Rage amesema ni kweli viongozi wa vilabu vya Tanzania hawana malengo ya kushinda vikombe vya kimataifa ikiwemo michuano ya Afrika na Dunia. Rage ameyasema hayo kufatia kauli aliyoitoa mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta kuwa 'vilabu vikubwa vya Tanzania havina mipango ya kushinda vikombe vya Afrika, wao mipango yao ni kushinda kombe la ligi na kumfunga mpinzani wake'. Katika kuthibitisha hilo Rage amesema kauli ya Mbwana ni ya kweli ndiyo maana vilabu vya Tanzania hutolewa mapema kwenye michuano ya Afrika kwasababu havijajipanga kushindana kimataifa. Rage akiongelea vilabu vya Simba na Yanga ambavyo ndiyo vikubwa, alisema 'mipango ya Simba ni kumfunga Yanga na kuchukua ubingwa, hivyo hivyo kwa upande wa Yanga, kitu ambacho kitaendelea kutufanya tuishie hapa hapa miaka nenda rudi'. Mwaka huu Tanzania imewakilishwa na Simba, na Azam FC kwa upande wa Tanzania bara pamoja na Mafunzo na Super Falcon kwa upande wa Zanzibar, lakini hadi sasa Tanzania imebakiza timu moja tu ya Azam FC ambayo wiki hii itacheza na AS FAR ya Morocco katika mchezo ambao utakuwa mgumu kwa Azam baada ya kutoka droo ya bila kufungana jijini Dar es salaam.
Nadal na Maria washinda Barcelona na Stuttgart
![]() |
Rafael Nadal (Kushoto) akiwa ameshikilia kombe aliloshinda katika michuano ya Barcelona open baada ya kumshinda mpinzani wake Nicolas (kulia) kwa seti mbili mfululizo 6-4, 6-3. Hii inakuwa ni mara ya nane kwa Rafael Nadal kushinda Barcelona open ikiwa ni michuano ya nyumbani akiwa kama raia wa Hispania. Nadal aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu ameanza kurudi kwenye kiwango chake licha ya kufungwa na Djokovic katika michuano iliyopita ya Monte Carlo. Nadal ameahidi kufanya vizuri zaidi kwenye michuano inayofuata ya French open ambayo yeye hujigamba kuwa ndiyo michuano yake akiwa anashikilia rekodi ya kushinda mara saba zaidi ya wenzake. |
Rekodi ya tuzo za PFA kuanzia mwaka 1973/74
1973–74 |
Norman Hunter - Leeds United
|
1993–94 |
Eric Cantona - Manchester Utd |
1974–75 |
Colin Todd - Derby County
|
1994–95 |
Alan Shearer - Blackburn Rovers |
1975–76 |
Pat Jennings - Tottenham H
|
1995–96 |
Les Ferdinand - Newcastle |
1976–77 |
Andy Gray - Aston Villa
|
1996–97 |
Alan Shearer - Newcastle |
1977–78 |
Peter Shilton - Nottingham F
|
1997–98 |
Dennis Bergkamp -Arsenal |
1978–79 |
Liam Brady - Arsenal
|
1998–99
|
David Ginola - Tottenham H
|
1979–80 |
Liverpool - FWA
|
1999–20
|
Roy Keane - Manchester Utd
|
1980–81 |
John Wark - Ipswich Town
|
2000–01
|
T Sheringham - Manchester Utd
|
1981–82 |
Kevin Keegan - Southampton
|
2001–02
|
Ruud van Nistelrooy- Manchester
|
1982–83 |
Kenny Dalglish - Liverpool
|
2002–03
|
Thierry Henry - Arsenal
|
1983–84 |
Ian Rush - Liverpool
|
2003–04
|
Thierry Henry - Arsenal
|
1984–85 |
Peter Reid - Everton
|
2004–05
|
John Terry - Chelsea
|
1985–86 |
Gary Lineker - Everton
|
2005–06
|
Steven Gerrard - Liverpool
|
1986–87 |
Clive Allen - Tottenham H
|
2006–07
|
C Ronaldo - Manchester
Utd
|
1987–88 |
John Barnes - Liverpool
|
2007–08
|
C Ronaldo -Manchester
Utd
|
1988–89 |
Mark Hughes - Manchester Utd
|
2008–09
|
Ryan Giggs - Manchester Utd
|
1989–90 |
David Platt - Aston Villa
|
2009–10
|
Wayne Rooney - Manchester Utd
|
1990–91 |
Mark Hughes - Manchester Utd
|
2010–11
|
Gareth Bale - Tottenham H
|
1991–92 |
Gary Pallister - Manchester Utd
|
2011–12
|
Robin van Persie
Arsenal
|
1992–93 |
Paul McGrath - Aston Villa
|
2012–13
|
Gareth Bale - Tottenham Hotspur
|
Gareth Bale ameshinda tuzo ya PFA
![]() |
Gareth Bale akiwa ameshikilia tuzo mbili za mchezaji bora wa mwaka PFA na nyingine ya mcheza bora kijana. Bale anaungana na wachezaji wachache ambao wameshawahi kuchukua tuzo hizi mara mbili akiwemo Cristiano Ronaldo, Mark Hughes, Alan Shearer na Thierry Henry. Mara ya kwanza Bale alishinda tuzo hii mwaka 2010-11 |
![]() |
Picha ya pamoja mchezaji bora wa kike Kim Little, mchezaji bora wa kiume Bale na mwenyekiti wa PFA Gordon Taylor (kushoto) |
Sunday, April 28, 2013
Azam FC wamepanda pipa leo kuelekea Morocco
Klabu ya Azam FC leo imesafiri kwenda nchini Morocco kucheza na AS FAR katika mchezo wa marudiano kwenye michuano ya washindi barani Afrika. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es salaam, Azam FC na AS FAR zilitoka droo ya bila kufungana hivyo basi Azam FC inatakiwa kutoka droo yoyote ya magoli au kushinda katika mchezo wake wa marudiano jijini Rabat. Azam FC wameondoka leo na ndege ya shirika la Emirate wakipitia Dubai ikiwa wachezaji wawili wamebaki akiwemo Nuhu Eliye ambaye ni majeruhi pamoja na Ibrahim Shikanda anayeelekea jijini Nairobi nchini Kenya kwenye masomo.
Jay Z ndani ya Emirates kuwatazama Arsenal
Rapa wa Kimarekani maarufu kwa jina la Jay Z leo alikuwepo
katika dimba la Emirates kutazama mechi kati ya Arsenal na Man utd, Jay Z alionekana
akiwa na Chris Martin wakitazama mechi iliyokwisha kwa timu hizo kutoka droo ya
goli moja kwa moja. Jay Z ambaye alianza kuishabikia Arsenal baada ya
kushawishiwa na Thierry Henry tokea mwaka 2010 baada ya Henry kuhamia kwenye
klabu ya New York Red Bulls nchini Marekani. Jay Z akiwa ni mwekezaji wa
michezo mbalimbali nchini Marekani amekuwa na nia ya kuwekeza kwenye ligi kuu
nchini Uingereza husani klabu ya Arsenal hadi sasa Jay Z anafanya tathimini
kabla ya kuwekeza kwa klabu hiyo.
Arsenal yapunguzwa kasi na Man utd
Timu za Arsenal na Man utd leo zimetoka droo ya goli 1-1
katika mchezo wa ligi kuu nchini England, Manchester United walishuka dimbani
kukamilisha ratiba kwani walishatangazwa mabingwa wa ligi hiyo wiki iliyopita
baada ya kushinda goli 3-0 dhidi ya Aston Villa. Lakini kwa upande wa Arsenal
mambo bado magumu wakiwa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi nne za juu
ili kupata nafasi ya ushiriki wa klabu bingwa ulaya (UEFA champions). Kwa
matokeo ya leo Arsenal wamefikisha pointi 64 wakiwa nafasi ya nne wakati
wapinzani wao Chelsea wameshinda mchezo wa leo na wamepanda hadi nafasi ya tatu
wakati Tottenham watacheza mechi yao ya 35 tarehe 4 May dhidi ya Southampton. Angalia msimamo
wa ligi ulivyo sasa ikiwa utamu wa ligi upo kwa timu hizi tatu za Chelsea,
Arsenal na Tottenham.
# | Team Name | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
1 | Manchester United | 35 | 27 | 4 | 4 | 79 | 36 | +43 | 85 |
2 | Manchester City | 34 | 21 | 8 | 5 | 61 | 31 | +30 | 71 |
3 | Chelsea | 34 | 19 | 8 | 7 | 68 | 35 | +33 | 65 |
4 | Arsenal | 35 | 18 | 10 | 7 | 66 | 36 | +30 | 64 |
5 | Tottenham | 34 | 18 | 8 | 8 | 60 | 43 | +17 | 62 |
6 | Everton | 35 | 15 | 14 | 6 | 52 | 38 | +14 | 59 |
7 | Liverpool | 35 | 14 | 12 | 9 | 67 | 42 | +25 | 54 |
8 | West Bromwich Albion | 34 | 14 | 6 | 14 | 46 | 44 | +2 | 48 |
9 | Swansea | 34 | 10 | 12 | 12 | 43 | 44 | –1 | 42 |
10 | West Ham | 35 | 11 | 9 | 15 | 41 | 49 | –8 | 42 |
11 | Fulham | 35 | 10 | 10 | 15 | 44 | 53 | –9 | 40 |
12 | Stoke | 35 | 9 | 13 | 13 | 31 | 41 | –10 | 40 |
13 | Southampton | 35 | 9 | 12 | 14 | 47 | 57 | –10 | 39 |
14 | Norwich | 35 | 8 | 14 | 13 | 33 | 54 | –21 | 38 |
15 | Sunderland | 34 | 9 | 10 | 15 | 38 | 45 | –7 | 37 |
16 | Newcastle United | 35 | 10 | 7 | 18 | 43 | 66 | –23 | 37 |
17 | Aston Villa | 34 | 8 | 10 | 16 | 36 | 63 | –27 | 34 |
18 | Wigan | 34 | 8 | 8 | 18 | 39 | 62 | –23 | 32 |
19 | Queens Park Rangers | 35 | 4 | 13 | 18 | 29 | 56 | –27 | 25 |
20 | Reading | 35 | 5 | 10 | 20 | 37 | 65 | –28 | 25 |
![]() |
RVP akiingia dimbani pembeni wakiwepo wahudumu wa ndege ya Fly Emirates wadhamini wakuu wa Arsenal ikiwa ni pongezi kwa wachezaji wa Man utd kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini England mwaka 2012/13 |
![]() |
Walcott akifunga goli pekee la Arsenal |
![]() |
RVP akifunga goli la kusawazisha kwa penati |
Subscribe to:
Posts (Atom)