Kocha wa Man utd Sir Alex Ferguson amemwambia Van Persie
kuwapuuza baadhi ya mashabiki wa Arsenal waliojipanga kumzomea kwenye mechi
kati ya Arsenal na Man utd itakayofanyika jumapili ya wiki hii. Ferguson
alisema ‘najua wapenzi wa Arsenal walichukia kumpoteza RVP aliyehamia United
hivi karibuni lakini haitakuwa vyema kumzomea mchezaji huo kwasababu alihama
kwa kufuata utaratibu, ila namtaka RVP kuwapuuza wote watakao mzomea'. Wakati
huo huo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amewataka mashabiki hao waliopanga
kuzomea wasifanye hivyo badala yake wampige makofi kuonesha heshima na
shukrani kwa RVP. RVP aliyefunga magoli matatu dhidi ya Aston Villa kwenye
mchezo uliopita, magoli yaliyoiwezesha United kutwaa ubingwa wa ligi
anatarajiwa kucheza katika mchezo huo wa jumapili ambao utakuwa ni mchezo
muhimu sana kwa Arsenal kushinda ili kujiimarisha katika nafasi tatu, vilevile
RVP atahitaji afunge goli au magoli dhidi ya timu yake ya zamani ili
kudhihirisha kiwango chake mbele ya mashabiki wa Arsenal wanaotaka kumzomea.
No comments:
Post a Comment